Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ally Salum Hapi, amefanya ziara ya kutembelea maghala ya chakula Serikali na binafsi pamoja na masoko ili kujiridhisha na hali ya chakula kwa Mkoa wa Dar es Salaam
Akizungumza mara baada ya ukaguzi alioufanya maeneo ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Kipawa NFRA, Ghala la Chakula na Nafaka Gongo Stores, Soko la Tandika, Soko la Buguruni, Soko la Tandale na Manzese kwa Msouth,
Aidha, Hapi amesema ameridhishwa na hali ya chakula kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kueleza kuwa chakula kipo cha kutosha ikiwemo Mchele, Mahindi, Maharage na vile vyakula vyote vya kilimo cha kijani na kusisitiza hakuna uhaba wa chakula na tetesi za njaa ni hadithi za kusadikika .
Hata hivyo, amewataka wakazi wa Dar es Salaam waendelee na shughuli za uzalishaji kwani wafanyabiashara wote wamemhakikishia kuwa chakula kipo na hawana desturi ya kuficha chakula.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Mkoa wa Dar es Salaam Elizabeth Mashote, amesema kuwa Dar es Salaam inatumia tani 2923 za chakula cha wanga kwa siku huku tani 530 zikiwa za vyakula vya protini na kusisitiza kuwa chakula kipo cha kutosha.