Mnamo mwaka 1808, gari la kwanza duniani liligunduliwa ambapo injini yake ilitengenezwa kwa mchanganyiko wa hidrojeni na oksijeni.

1st-car-3-wheels

Aliyegundua gari hilo alijulikana kwa jina la Isaac De Rivaz raia wa Ufaransa na Uswiz, hata hivyo aina hiyo ya gari alilogundua haikufaulu katika matumizi yake, Pia wagunduzi wa Kimarekani, Samuel brown na Samuel Murray walishindwa kufaulu vizuri kama mgunduzi wa kwanza.

François Isaac de Rivaz

François Isaac de Rivaz (Desemba 19, 1752 – Julai 30, 1828)

Baada ya miaka 24, Entiene Noire alifanikiwa kutengeneza injini  lakini baada ya kuiweka kwenye gari ilikuwa ikifanya kazi taratibu kuliko hata binadamu. Mnamo mwaka 1886 Januari 26, Mgunduzi wa Kijerumani  aligundua gari aina ya Karl Benz yenye ‘gasoline auto motor’ huko Ujerumani, na Karl Benz ndiye aliyekuwa wa kwanza kuanzisha msingi wa viwanda vya magari ya aoutomatic duniani, alitengeneza gari yenye matairi matatu kama gari ya kihistoria jijini kwake ‘roam’.

Karl Benz

Baada ya hapo Gottlieb Daimler aligundua gesi na kutengeneza gari lake kwa kutumia hiyo gesi. Mwaka huo huo Machi, aina hiyo ya gari kwa mara ya kwanza ilitengenezwa yenye matairi manne, yenye enjini inayotumia mafuta mengi na ilikuwa tayari kutangazwa.

1889 Daimler alitambulisha injini mpya na baada ya mwaka mmoja Daimler aliitangaza rasmi Daimler kama kampuni yake mpya ya uzalishaji magari aina ya Daimler huko Ujerumani katika mji wa Stuttgart ili kuanza ushindani na makampuni mengine ya uzalishaji magari.

                           daimler-motorkutsche-auto-100-_v-img__16__9__l_-1dc0e8f74459dd04c91a0d45af4972b9069f1135

Gottlieb Wilhelm Daimler

Gottlieb Wilhelm Daimler

Kurasa za WhatsApp kuanza kurusha matangazo 2020
Serikali: Hakuna mgonjwa wa ebola Tanzania