Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu 24 za makundi A, B, C na D kucheza  katika viwanja 12 mbalimbali nchini, kusaka nafasi nne za kupanda Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao (StarTime First League).

Kesho Jumamosi Kundi A, Mvuvuma FC watakua wenyeji wa Abajalo FC ya Tabora  uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Transit Camp watacheza dhidi ya Mirambo FC uwanja wa Kamabarage Shinyanga, huku Singida United watawakaribisha Green Warriors katika uwanja wa Namfua mjini Singida.

Kundi B, Allicane FC watawakaribisha AFC ya Arusha uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma watacheza dhidi ya Madini FC uwanja wa Karume Musoma, Kundi C, Changanyikeni dhidi ya Karikoo ya Lindi watacheza katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Mechi hizo zitaendelea kwa Kundi D, ambapo African Wanderes watawakaribisha Sabasaba FC uwanja wa Wambi, Mafinga, Mkamba Rangers dhidi ya Mbeya Warriors uwanja wa CCM Mkamba, na Wenda FC watacheza dhidi ya Mighty Elephant uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo mitatu kuchezwa katika kundi B, na C, Pamba FC watawakaribisha Bulyanhulu FC uwanja wa CCM Kirumba, Mshikamo dhidi ya Abajalo uwanja wa Mabatini, Mlandizi na Villa Squad kuchuana dhidi ya Comsopolitan uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Rais Amsimamisha Kazi Kamishna Mkuu wa TRA
Milionea Aliyemuua Mtu Aliyempiga Picha Mwanae Wa Kike Asamehewa Kwenda Jela