Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli, 25, atakataa kujiunga na Lazio au Sampdoria kwa mkopo kwa sababu atalipwa fedha nyingi tu za ‘uzalendo’ kama bado atakuwepo Anfield dirisha la uhamisho likifungwa (Daily Mirror)

Juventus wanafikiria kumchukua kiungo wa Liverpool Lucas, 28, ambaye hakutajwa kwenye kikosi cha Brendan Rodgers dhidi ya Stoke wiki iliyopita (Daily Express)

Matumaini ya Manchester United kumsajili beki wa Real Madrid Sergio Ramos, 29, yamekwisha baada ya beki huyo kujiandaa kuongeza mkataba wake wiki ijayo (Guardian)

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema ana matumaini kuwa mshambuliaji Wayne Rooney, 29, ataweza kupachika mabao zaidi ya 20 msimu huu (Independent)

Mshambuliaji wa Tottenham, Roberto Soldado, 30, amesafiki kwenda Spain kukamilisha uhamisho wake kwenda Villareal (Guardian)

Emmanuel Adebayos, 31, wa Tottenham na Javier Hernandez wa Manchester United, 27, ni kati ya washambuliaji wanaonyatiwa na West Ham (London Evening Standard)

Everton wanamtaka beki wa zamani wa kushoto wa Manchester United Alexander Buttner, 26, kuziba nafasi ya Leighton Baines aliyeumia (Daily Mail)

FIFA imemshutumu meneja wa Chelsea Jose Mourinho kwa jinsi alivyofarakana na daktari wa timu Dr Eva Carneiro (Daily Telegraph)

Sunderland wamekuwa na mazungumzo ya kumsajili tena mshambuliaji Fabio Borini kwa mkopo, mwaka mmoja baada ya mchezaji huyo kukataa kwenda Stadium of Light (Sunderland Echo)

QPR wanakaribia kumsajili beki wa Bolton Tim Ream, 27 (NBC Sports).

Waziri Mwingine Aanguka Kura Za Maoni, Slaa Apeta Ukonga
Baines Nje Majuma 12-13