Msanii wa muziki wa bongo fleva Rajbu Kahaliu maarufu Harmonize amesema kuwa atawafikisha Mahakamani wote ambao wanadaiwa kuvujisha picha, video na sauti siziso na maadili kwa lengo la kumchafua na kumdhalilisha.

Harmonize amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram Instagram ambapo amekana tuhuma hizo kwa kusema sio yeye kwenye picha na video hizo, pili atawafikisha Mahakamani wote waliohusika.

“Taarifa kwa Umaa, video zilizotengenezwa na kusambazwa mtandaoni zikiwa zinaonyesha sura yangu na kuunganishwa na utupu wa mtu mwingine kisha kuunganishwa na sauti yangu kwa lengo la kunichafua kunidhalilisha na kuharibu brand ambayo nimeitengeneza kwa mabilioni ya shilingi” ameandika Harmonize

“Sitaki kujua aliyetengeneza ni nani au kaipataje ila ninachosema ni kwamba yeyote aliyehusika na hili suala linalolenga kunichafua na kunidhalilisha lazima watafikishwa mahakamani ili kukomesha chuki na tamaa zinazoathiri watu wasio kuwa na hatia,  watanilipa fidia kubwa na ikiambatana na kifungo” ameongeza

Onyango: Mapambano yanaendelea VPL
Tarimba: Young Africans fuateni nyayo za Simba