Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Rajab Abdul maarufu Harmonize kwa mara ya kwanza ameonyesha picha za mtoto wake wa kwanza wa kike ambaye amemtambulisha kwa jina la Official Zulekha Kondegirl aliyempata mzazi mwenzake aliyemtaja kama Official Nana Shanteel.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize ameandika: “Kweli humuweka yeyote huru haijalishi ni kiasi gani au muda gani ila naamini kusema hili litafanya moyo wangu uwe huru na nijione muungwana mbele ya Mungu na wewe unayesoma, pia muungwana zaidi mbele ya mtoto wa wangu kipenzi Zuu, nianze kusema samahani kwa kutojivunia wewe kwa mwaka mmoja na miezi 7” 

“Nisamehe pia kwa kutokuwa na ‘time’ hata ya kuja kukuangalia pale ulipokuwa unaumwa, kwa kuhofia kuvunja mahusiano ambayo nayaheshimu sana, tumepitia mengi na naamini kuchezea wanawake au kubadili sio sifa, hili suala limenitesa kwa muda rrefu, hadi ikafika pahala nikasema namuachia Mungu” 

“Nakuomba msamaha hadharini na nakuahidi kukupa moyo wangu wote, kwani hukuja kwenye hii dunia kwa bahati mbaya ni mpango wa Mungu nakupenda malkia wangu umenifanya nijione mtu mzima, nimejifunza na natarajia kujifunza mengi  kupitia wewe Official Zulekha Kondegirl, nilishasema ‘privately’ na nasema tena hadharani nisamehe mke wangu nina imani utalipokea kibinadaam” ameandika Harmonize.

Kwa upande wake mke wa Harmonize, Sarah Michelotti kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha zinazoonesha vipimo vya DNA na kuandika:

“Mungu wangu watu kweli wamevurugwa, mara mbili wamepima DNA ya mtoto bado majibu ni Negative., Ila kwakua umeshindwa kupata mtoto umeamua kujipa mtoto asie wako….hongera kwa adoption, utakua na roho nzuri, hukujua jinsi ya kutunza mke sababu ya maovu yako natumai utajua kutunza mtoto…, UKOME KUONGOPEA MASHABIKI ZAKO. Dah 🙏 I post it in swaili language, so everybody will understand 👌” ameandika Sarah.

Harmonize na Sarah wamekuwa katika mahusiano kwa karibu miaka mitatu na walifunga ndoa Septemba 2019 (Takriban mwaka mmoja na miezi mitatu iliyopita), suala ambalo linaonyesha mtoto huyo alizaliwa wakati wawili hao wakiwa tayari katika mahusiano.

Plateau United kutua Dar leo
Lwandamina kuifuata Azam FC Mwanza

Comments

comments