Mwanamuziki maarufu wa Bongo Flava, Harmonize ameweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake Briana, raia wa Australia kwa sasa hawapo pamoja kwenye mahusiano kufuatia uamuzi aliochukua wa kumrudia mwanamke anayedai kumpenda kwa dhati.

Konde boy ameyasema hayo huku akionesha viashiria vya kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni muigizaji maarufu nchini, Kajala Masanja

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta Stori), Harmonize amesema kuwa hana tatizo lolote na mrembo Briana ila kwa sasa hawapo pamoja kutokana na sababu mbili kuu.

“Nilimwambia Briana kuwa nimetengana na mtu bila kugombana na nampenda sana, sina uhakika kama nime-move on, lolote linaweza kutokea maana itakuwa ni kitendo cha kizalendo mimi kurudi nyumbani.”

Ameandika Harmonize akiitaja hiyo kama sababu ya kwanza na kuendelea kwa kusema nyingine ni kwamba mrembo huyo raia wa Australia hakuwa tayari kuishi nchini Tanzania kitendo ambacho yeye hakikumvutia kwa madai ya kuwa hata yeye bado hajafikiria kwenda kuishi Australia.

Harmonize ametilia mkazo kuwa kwa sasa anachohitaji ni mke wake arejee kwanza halafu mambo mengine ndio yafuate.

Makamu wa Rais kuzindua mbio za mwenge April 2
Kocha Simba SC aiota US Gendarmerie