Rajab Abdul Kahali Maarufu kama Harmonize amefunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Sara,wawili hao wamefunga ndoa ya kiislamu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 7,2019.

Mkali huyo wa ‘Inabana’ aliahidi kufunga ndoa na mchumba wake huyo pindi tu alipomvalisha pete mapema mwaka huu.

Sara na Harmonize imekuwa ‘couple’ maarufu nchini tangu walipokutana, huku akimuweka kwenye baadhi ya video za nyimbo zake.

Katika hatua nyingine, Mwanamuziki mkongwe, Nguza Viking maarufu Babu Seya naye amefunga ndoa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Muheza (DAS), Esterine Haule. Wawili hao wamefunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki la Sinza Jijini Dar es Salaam.

Babu Seya ambaye wimbo wake maarufu ‘Seya’ ulimpa mashabiki wengi nchini, amefanikiwa kupata furaha yake tena ikiwa ni takribani miaka miwili tu tangu yeye na mwanaye Papii Kocha, walipoachiwa huru kutoka gerezani kwa msamaha wa Rais, John Magufuli.

 

 

 

 

Mchekeshaji Kevin Hart afanyiwa upasuaji
Maghembe aiomba Serikali kuingilia kati wizi wa vifurushi vya simu