Hatimaye Harmonize ameanika jinsi alivyoachana na menejimenti ya WCB na kuanzisha biashara yake binafsi, akidai kuwa anaendelea kuhangaika kulipa deni la Sh  milioni 500 ili akidhi masharti ya kuvunja mkataba.

Mwimbaji huyo amefunguka leo kwenye XXL ya Clouds FM, ameeleza kuwa baada ya kuona hawezi kuendelea na uongozi wa WCB kutokana na kuwepo matatizo ambayo hakuyaweka wazi, aliamua kuomba ridhaa kwa uongozi huo ili aanzishe kibanda chake.

Amesema uongozi huo ulipokea ombi lake kwa mtazamo chanya lakini ukamwambia afuate taratibu zilizoainishwa kwenye mkataba wao wa awali, kabla ya kumtengeneza kuwa Harmonize.

“Waliniambia kama nataka kutoka inabidi nifuate masharti ya mkataba ambao tuliandikishana kabla sijawa Harmonize, ambao ulikuwa unaeleza kuwa kama nataka kuvunja mkataba ilinibidi nilipe Sh milioni 500 na gharama ya nyimbo zote zilizotengenezwa wakati niko pale,”amesema Harmonize.

Mwimbaji huyo amdai kuwa ili kukamilisha sharti hilo, ilimbidi auze baadhi ya mali zake ikiwa ni pamoja na nyumba tatu alizokuwa anajenga na kwamba tayari wameshalipa sehemu kubwa ya deni hilo.

Konde Boi ambaye leo ameachia wimbo mpya ‘Uno’amekiri kuwa uongozi wa WCB ulimkataza kutumia nyimbo alizorekodi akiwa mikononi mwao hadi pale atakapokamilisha masharti ya kuvunja mkataba. Hivyo, atakapokamilisha kulipa deni la Sh. 500 Milioni na kulipia baadhi ya gharama atakuwa huru kuendelea kutumia nyimbo hizo.

Ameeleza kuwa ameamua kufuata utaratibu huo kwa sababu anaamini fedha sio kila kitu na kwamba WCB ni leobo iliyompa mafanikio hivyo angependa waendelee kuwa na urafiki wa kibiashara.

Harmonize asimulia alivyopokea simu ya Rais Magufuli usiku, aahidi kuwa mbunge
Hamisa Mobetto avuka mipaka kwa mama yake mzazi