Msanii wa bongo fleva, Harmonize amewatolea uvivu wanaosambaza uvumi wa kuwa wimbo aliomuimbia Said Salim Bakhresa ni sawa na tangazo la bure kwa tajiri huyo na kuwa anajisogeza karibu kwa mfanyabiashara huyo maarufu Afrika mashariki.

Harmonize ameeleza wazi dhamira yake kuu ya kuimba wimbo huo kuwa ni kuwavutia vijana kujituma ili kupata maendeleo.

“MY MUSIC  IS MORE ABOUT LIFE & PEOPLE Binafsi Nitafarijika zaidi kuona watu wakibadilisha mwenendo wa maisha kupitia wimbo huu, nitafarijika sana kumuona kijana mwenzangu yeyote mtaani mwenye kipato kidogo akiutumia huu wimbo kama wake up call na kumtazama Bakhresa Kama mfano wa wazi,” amesema Harmonize.

Ameongeza kuwa atafurahi akiona kijana anaanza, kuzifuata ndoto kubwa zaidi

“nitafarijika kuona hakuna kudharauliana tunaishi kwa heshima na usawa bila kujali hapa Instagram una followers wangapi, Maisha ya Bakhresa ni mfano bora wa kuigwa ingawa sio lazima kila tajiri aishi kama anavyoishi Bakhresa,”

“Nimalize kwa kusema MZEE BAKHRESA KUSIKIA WIMBO HUU haitokuwa ni jambo la ajabu kwake kwasababu niliyoyasema yote anafanya, mafanikio niliyoyataja yote anayo na bila shaka haya ni machache tuu, kama angetaka kuimbwa basi angemlipa hata DRAKE.”

Maaana uwezo huwo bila shaka anao, binafsi sina haja kabisa ya mzee Bakhresa kuusikia wimbo huu maana ningetaka hivyo basi ningefanya utaratibu wa kuitafuta familia yake ndugu, Jamaa na Marafiki ili wimbo umfikie asikilize kama lengo lilikuwa ni kumsifia, kifupi sina urafiki au ukatibu wowote na ndugu wa mzee Bakhresa lengo langu kubwa.

Huu wimbo ukufikie wewe masikini mwenzangu uliyenyanyasika na masikini wenzako ambao wanakuzidi kipato kidogo tu, upate nguvu na uamke tena, wimbo huu ukufikie wewe mwenye ndoto ndogo uavhane nayo utafute kubwa zaidi

Mwisho we thank God for the life of big boss Bakhresa, PIA WALE MNAOSEMA NIMEFANYA TANGAZO LA BURE, NI WAKATI WAKUWAKUMBUSHA MATAJIRI WENGINE WAYAFANYE MEMA YA KUMPENDEZA MUNGU NA BINADAMU ILI WAPATE MATANGAZO YA BURE KAMA HAYA.”

Harmonize ameyasema hayo kwa njia ya maandishi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram mapema Machi 12, 2022.

Moto wateketeza kiwanda cha GSM
Rich Mavoko ajinadi upya