Kasi ya kufumania nyavu ya Bayern Munich hasa kwa mshambuliaji Harry Kane hapana shaka inaiweka katika presha kubwa Manchester United wakati timu hizo zitakapokutana kwenye mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika Uwanja wa Allianz Arena jijini Munich leo Jumatano (Septemba 20).

Wakati wageni wakiingia katika mchezo huo wa leo Jumatano (Septemba 20) ambao wa kwanza kwa kila timu kwenye Kundi A wakiwa na mwenendo mbaya katika siku za hivi karibuni huku safu yao ya ulinzi ikiwa taabani, Bayern Munich wenyewe wamekuwa moto wa kuotea mbali hasa katika kupachika mabao, jambo linaloilazimisha Manchester United kufanya kazi ya ziada ili iweze kuvuna pointi tatu katika mechi hiyo.

Katika mechi tano za mashindano ilizocheza msimu huu, Bayern imefunga mabao ll ikiwa ni wastani wa mabao 2-2 kwa mchezo ingawa safu yake ya ulinzi nayo imekuwa na udhaifu ikiruhusu mabao saba saa na wastani wa bao 14 kwa mchezo.

Kana kwamba haitoshi, Bayern Munich imekuwa na historia tamu nyumbani pindi inapoikaribisha Man United ambapo katika mechi tano zilizopita ambazo ilikuwa mwenyeji dhidi ya timu hiyo, ilipata ushindi mara tatu na kutoka sare mara mbili.

Lakini ukiondoa makali hayo ya Bayern kufumania nyavu kama timu, nyota wake Harry Kane ambaye amekuwa moto wa kuotea mbali tangu alipojiunga nayo katika dirisha la majira ya kiangazi akitokea Tottenham Hotspur ambapo katika mechi nne alizoichezea kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani hadi sasa, amepachika mabao manne ikiwa ni wastani wa bao moja katika kila mchezo.

Mshambuliaji huyo pia katika mechi 10 zilizopita alizokutana na Manchester United, amehusika na mabao saba akifunga mabao manne na kupiga pasi tatu za mwisho.

Kw a wageni, wanaingia katika mchezo huo wakiwa hawapo vizuri kwani wamefunga mabao sita tu katika mechi zao tano zilizopita za Ligi Kuu England huku nyavu zao zikitikiswa mara 10 na wameshinda mechi mbili tu kati ya hizo huku wakipoteza tatu.

Mechi hiyo ya leo Jumatano (Septemba 20) itachezeshwa na Mwamuzi Glenn Nyberg ambaye atasaidiwa na raia wenzake wa Sweden, Mahbod Beigi, Andreas Söderkvist na Adam Ladeback.

Jjini London katika Uwania wa Emirates, wenyeji Arsenal baada ya kukaa kwa miaka sita bila kucheza Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, leo Jumatano (Septemba 20) watakuwa na kibarua mbele ya PSV ya Uholanzi.

Kocha Dabo hataki ugaigai Azam FC
Mbaroni kwa kumjeruhi Dada wa kazi kwa Chai