Mshambuliaji Harry Kane wameshinda rufaa na kuzawadia bao la pili la Tottenham Hotspur dhidi ya Stoke City.
Chama cha soka nchini England (FA), waliidhinisha bao hilo la ushindi kwa Spurs kuwa hali kwa Christian Eriksen kutokana na maelezo ya mchezo huo walivyoyapokea, hali ambayo ilimlazimu Harry Kane kwa kushirikiana na voingozi wake kukata rufaa na kuomba kurudiwa kwa picha za televisheni ili kubaini ukweli wa nani alifunga.
Katika taarifa iliyotolewa na FA imeeleza kuwa, Harry Kane aliugisa mpira wa adhabu iliyopigwa na Christian Eriksen kabla ya kuingia wavuni, hivyo wamejiridhisha mshambuliaji huyo kuwa na haki.
Maamuzi hayo yanamfanya Harry Kane kufikisha mabao 25 aliofunga katika michezo ya ligi kuu msimu huu, na sasa anakua nyuma kwa mabao manne dhidi ya mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu.
Kane bado ana matumaini makubwa ya kumfikia mshambuliaji huyo kutoka nchini Misri, kabla ya kufikia mwishoni mwa msimu huu.