Nahodha na Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane amesisitiza inapaswa kuona Klabu hiyo inapaswa kushiriki Michuano ya Ligi ya Europa kama nafasi ya kumaliza ukame wa mataji klabuni hapo kwa msimu ujao 2023/24.
Spurs wana nafasi ya kucheza mashindano ya Ulaya baada ya ushindi wa bao 1-0 Jumamosi (Mei 06) dhidi ya Crystal Palace ambapo bao la kichwa la kipindi cha kwanza la Kane liliisaidia kupanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Brighton, walio katika nafasi ya saba, bado wanapewa nafasi kubwa ya kufuzu Ligi ya Europa ikizingatiwa wana mechi tatu mkononi na wamepitwa alama mbili na Tottenham.
Nahodha huyo wa kikosi cha Timu ya Taifa ya England amesema: “Tumebakisha mechi tatu, mchezo mkubwa ni dhidi ya Villa wiki ijayo ugenini.”
“Ni wazi kwamba Brighton wana me- chi chache mkononi kwetu. Ikiwa tunaweza kuondoka msimu huu na soka la Ulaya, hiyo ni tuzo muhimu kwetu.”
“Tutapigania hilo na kupigana katika mechi tatu kujaribu kupata ushindi mara tatu.”
“Mwisho napenda kucheza michezo ya mpira wa miguu bila kujali ni mashindano gani. Hicho ndicho unachostahili kutoka pale unapomaliza msimu.”
“Huwezi kudharau mashindano yoyote ambayo unacheza. Ni mojawapo ya hayo, ikiwa utaishia kwenye Ligi ya Europa Conference ni sawa.”
“Lakini unapokuwa katika klabu ambayo hatujashinda kombe kwa miaka 15, ikiwa tutaishia humo, inaweza kuwa fursa nzuri.”
Bao la 209 la Kane kwenye Ligi Kuu England lilimaliza mechi ngumu na Palace baada ya Tottenham kusawazisha kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu tangu Februari 26.