Hatima ya kiungo wa zamani wa Yanga Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ya kurejea Jangwani sasa ipo mikononi mwa Kocha Mkuu Mkongomani, Mwinyi Zahera.

Kiungo huyo anakipiga Klabu ya AS Kigali ya nchini Rwanda baada ya mkataba wake wa kuichezea Simba kumalizika na kuamua kurudi nyumbani kwake kucheza soka.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi na kuthibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, jukumu la usajili lipo kwa kocha wao Zahera ambaye ndiye anapendekeza usajili na siyo viongozi.

Mwakalebela alisema kuwa kama kocha akimhitaji kiungo huyo, basi wao hawatakataa mapendekezo yake na watamsajili kama ilivyokuwa kwenye usajili uliopita.

“Tutasikiliza maoni ya kocha kama akitupa mapendekezo yake ya kumsajili, basi kama uongozi hatutasita kumsajili kiungo wetu wa zamani aliyecheza kwa mafanikio muda mrefu”.

“Ipo wazi Niyonzima ameitumikia kwa kipindi kirefu tangu mwaka 2012 alipojiunga na Yanga, akiwa hapa aliitumika Yanga kwa mapenzi yote na alifurahia uwepo wake katika timu” amesema Mwakalebela

Hiyo imejiri ikiwa ni siku chache tangu kiungo huyo atoe ya moyoni kuwa yupo tayari kurejea kukipiga Yanga kama timu hiyo ikihitaji huduma yake kwenye dirisha dogo la usajili.

Dalili za kujiua, 'Wanaume vinara, wanawake huongoza kwa kufanya majaribio'
Lil Ommy ashinda tuzo ya Mtangazaji Bora Afrika, Diamond, Nandy, Ray Vanny nao wabeba