Watu zaidi ya 100 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 150 wamejeruhiwa nchini Iraq, baada ya kuzuka kwa moto ndani ya ukumbi wa harusi katika mkoa wa Kaskazini wa Nineveh.

Naibu Gavana wa Mkoa huo, Hassan al-Allaq amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa moto huo ulianza saa nne usiku wakati watu hao wakiwa kwenye sherehe ya harusi.

Kutokana na hali ya majeruhi ilivyo, al-Allaq ameonya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya watu waliopoteza maisha ikaongezeka huku walioshudia wanasema wageni waliokuwa wamealikwa kwenye sherehe hiyo, walikuwa kwenye burudani wakati moto mkubwa ulipozuka ghafla.

Hata hivyo, Maafisa wa ukoaji wameonekana wakiuzima moto huo na kuwatafuta manusura ambao wamekimbikizwa hospitalini huku taarifa za awali zikisema moto huo ulitokana na fataki zilizorushwa kwenye ukumbi huo.

Putin agoma kupoa vita ya Urusi, Ukraine
Taaluma ya Madini: GGML yawanoa Wanafunzi Nyankumbu