Afisa Habari wa Azam FC Hasheem Ibwe, amesema kuwa wanaoibeza timu hiyo watakutana na balaa kwenye ligi na mashindano mengine.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo, iligotea nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Ngao ya Jamii ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate, watupiaji wakiwa ni Prince Dube na Abdul Suleiman Sopu.

Akizungumza baada ya kikosi chao kurejea jijini Dar es salaam, Ibwe amesema wapo ambao walikuwa wakisema timu hiyo haina ubora, lakini kupitia mchezo wa pili waliona picha halisi.

“Kupoteza mchezo wa kwanza wa Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans haina maana kwamba hatuna kikosi imara. Bahati nzuri kulikuwa na mechi ya pili iliyokuja na picha tofauti na waliokuwa wanabeza wameona ubora uliopo.

“Tunahitaji kufanya vizuri kwenye mashindano ambayo tunashiriki, hilo lipo wazi, tutapambana kufanya hivyo na mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi kwenye kila hatua,” amesema lbwe.

Lori la Mafuta lakamatwa likisafirisha wahamiaji haramu 65
Skudu kurejea mzigoni Young Africans