Mtanzania anayecheza mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Hasheem Thabit ametolewa uwanjani baada ya kufanya madhambi mara mbili.

Hasheem anapambana kwa sasa ili kuweza kurejesha ndoto zake za kucheza ligi kuu ya NBA, lakini amekuwa akipokea ushauri kutoka kwa wadau wa mchezo huo wa kumtaka kuelekeza fikra zake katika nchi nyingine kutokana na umri kumtupa mkono.

Hasheem alifanya madhambi mara mbili katika mchezo wa D League, ambao ulishuhudia kikosi cha Washington Wizards kikipambana.

Muamuzi wa mchezo huo alionyesha ishara kwa mchezaji huyo, kwa kuujulisha umma uliokua unashuhudia mpambano huo ni vipi alivyofanya makossa ambayo yalistahili kumpeleka nje ya uwanja.

Mdau wa michezo nchini Marekani, Chris Vivlamore aliandika katika ukurasa wake wa Twitter, sekunde chache mara baada ya Hasheem kuamuriwa kutoka nje ya uwanja maandishi ambayo yalionekana kama kejeli kwa mchezaji huyo wa kibongo.

Aliandika “Hasheem Thabeet, anayecheza D-League, amefanya madhambi mara mbili na kutolewa nje ya uwanja, na sasa yupo kwenye vyumba vya kubadilishia akipiga mabenchi pamoja na locker (Makabati).”

Young Killer Kuziweka Ngoma 14 Kwenye Mixtape Mpya
Klabu Ya Ulaya Yawaumbua Simba Kuhusu Emmanuel Okwi