Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wananchi wa vijiiji vya Iputi na KetaKeta wilayani Ulanga mkoani Morogoro kuwa wavumilivu wakati wanasubili wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoka  Ofisi ya Mkurugenzi wa ramani kwenda kusoma ramani ili kuweza kubaini mipaka halisi baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba la Selous.

Amesema kuwa migogoro ya mipaka kati ya Selous na vijijji hivyo hakuna mwenye dhamana ya kuonyesha mipaka hiyo  kwa vile wote ni wanaufaika.

“Selous wanatamani wawe na eneo kubwa zaidi kwa ajili ya wanayamapori vivyo hivyo Wanavijiji nao wanatamani wawe na eneo kubwa zaidI ajili ya shughuli za kilimo hivyo hakuna atakayeshinda’’ amesema Waziri Hasunga

Aidha, hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mipaka inapowekwa kwenye hifadhi lazima wawepo viongozi wa Vijiji, baadhi ya wazee wa vijiji pamoja na uongozi wa wilaya wakishuhudia uwekaji wa mipaka hiyo kutoka kwa wataalamu wa ofisi ya Mkurugenzi wa Ramani.

Ameyasema hayo wilayani Ulanga mkoani Morogoro alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Iputi na Katekate.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ulanga, Goodluck Milinga amesema kuwa mipaka ya maeneo ya vijiji hivyo imekuwa ikihamishwa hamishwa hali inayopelekea kuleta manung’uniko kutoka wananchi wake.

 

RC Hapi asmikwa rasmi kuwa Chifu wa Wahehe
Video: Ngome ya Lowassa Monduli yavunjika, Maalim Seif, Lowassa watikiswa