Mshambulaiji hatari wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Fiston Kalala Mayele amefunguka na kueleza alivyokua anajihisi kwa kushinda kuifungia klabu hiyo kwa michezo kadhaa iliyopita.
Mayele alishindwa kuifungia Young Africans katika michezo mitano mfululizo iliyopita, hali ambayo iliibua taharuki kwa Mashabiki wake na wale ambao wanafuatilia Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.
Mshambuliaji huyo kutoka DR Congo amesema alikua anajihisi vibaya kwa sababu jukumu lake kubwa ni kuisaidia timu kupata ushindi, na yeye amekua akitazamwa kama mkombozi kwa kuifungia Young Africans.
“Mimi kama Mshambuliaji huwa ninapambana kila mchezo niweze kufunga, ikitokea ninashindwa kufunga huwa sijihisi furaha kabisa, lakini nilikua ninaamini ipo siku nitafunga na leo (Jana) nimefanikiwa kufunga.” Amesema Mayele
Mayele alifunga mabao matatu pakee yake ‘HAT TRICK’, huku bao lingine likifungwa na Beki wa Kulia Shomari Kibwana na kuifanya Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
atua ya kuifungia Young Africans mabao matatu jana Alhamis (Novemba 17) dhidi Singida Big Stars inamuwezesha Meyele kufikisha mabao Sita msimu huu, sawa na Mshambuliaji wa Simba SC Moses Phiri, huku Sixtus Sabilo akiwa kileleni kwa kupachikwa mabao Saba.