Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp atakuwa na maisha yenye kuhitaji uvumilivu wa kutosha, kufuatia mastaa wake sita wa kikosi cha kwanza kufikiria kuachana na maisha ya Anfield mwishoni mwa msimu huu kutokana na mikataba yao kufikia ukingoni.

Staa mmoja tayari imeshathibitishwa kwamba ataondoka, Roberto Firmino atakayeachana na maisha ya Anfield baada ya miaka minane na kumduwaza Meneja Klopp.

Kuna mastaa wengine watano wa kikosi cha kwanza, akiwamo Alex Oxlade-Chamberlain wataondoka.

Habari njema kwa Klopp ni kuhusu Joe Gomez, Diogo Jota na Curtis Jones kwamba wote wameongeza mikataba yao na wataendelea kubaki kwenye kikosi hicho hadi 2027. Lakini, Klopp kijasho kitamtoka kwa wachezaji wanaopanga kuondoka, huku ikielezwa hali halisi ya mikataba ya wachezaji hao wa Anfield ilivyo.

Nani amebakiza muda gani Anfield.

Hii hapa orodha ya mastaa wa kikosi cha kwanza cha Liverpool na muda wa mikataba yao iliyobaki kwenye mabano.

Makipa: Alisson (2027), Caoimhin Kelleher (2026) na Adrian (2023)

Mabeki: Joe Gomez (2027), Calvin Ramsay (2027), Andy Robertson (2026), Ibrahima Konate (2026), Rhys Williams (2026), Virgil van Dijk (2025), Trent Alexander-Arnold (2025), Kostas Tsimikas (2025), Nat Phillips (2025) na Joel Matip (2024)

Viungo: Stefan Bajcetic (2027), Fabinho (2026), Jordan Henderson (2025), Thiago (2024), Naby Keita (2023), James Milner (2023), Alex Oxlade-Chamberlain (2023), Arthur (2023, mkopo)

Washambuliaji: Darwin Nunez (2028), Cody Gakpo (2028), Luis Diaz (2027), Fabio Carvalho (2027), Diogo Jota (2027), Mohamed Salah (2025), Roberto Firmino (2023).

Wapiga kelele makazi ya watu kuchukuliwa hatua
Young Africans yapiga hesabu kali Kwa Mkapa