Mahakama Wilaya ya Iringa leo inatarajia kusoma hukumu ya kesi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo.
Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, mwaka huu akiwa eneo la Ubungo, Dar es Salaam na kuzisambaza kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwamba yupo hatarini.
Katika shtaka la pili, anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga alipokuwa anatoa taarifa kwa askari kwenye Kituo cha Polisi Mafinga kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam na kupelekwa Kiwanda cha Pareto Mafinga.
Hata hivyo, katika kesi hiyo Nondo anatetewa na mawakili wawili wakiongozwa na Jebra Kambole chini ya mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini (THRDC).
-
Waziri Mkuu amjulia hali Waziri Kigwangalla
-
Ulega atoa maagizo mazito kuhusu tozo za Samaki
-
Lugola akomaa na wavamizi wa Ardhi