Wapiganaji wa Hamas wamewaachia huru mateka 24 Novemba 24, 2023 katika siku ya kwanza ya kusitishwa vita hivyo kwa mara ya kwanza tangu kusuasua kwa utekelezaji wa zoezi hilo muhimu.
Mateka hao wanatajwa kuwa ni Wanawake na watoto na Wafanyakazi wa Thailand na mmoja wa Ufilipino, baada ya silaha kunyamazishwa kwa mara ya kwanza kote Ukanda wa Gaza katika kipindi cha wiki saba.
Inaarifiwa kuwa Mateka hao walihamishwa kutoka Gaza na kukabidhiwa maafisa wa Misri katika kivuko cha Rafah, wakiandamana na wafanyakazi wanane wa Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu.
Hamas imewaachia mateka hao 24 iliyowashikilia Gaza kwa wiki kadhaa, na Israel ikawaachia wafungwa wa Kipalestina kutoka jela katika awamu ya kwanza ya mabadilishano chini ya mpango wa usitishwaji mapigano kwa siku nne.