Kufuatia kikao kilichofanyika jana kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri, Harrison Mwakyembe, Naibu wake, Juliana Shonza katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania, Godfrey Mwingereza na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisso na mwanamuziki Diamond Platinum pamoja aliyefuatana na mameneja wake.
Mapema leo hii Kwa Pamoja Wizara, Basata na Wasanii wamefikia muafaka wa Kuzifungulia nyimbo ambazo zilifungiwa hapo awali na wamekubaliana kujadili ni jinsi gani kwa pamoja wataweza kulinda maadali ili kusiwepo na poromoko la maadili kutokana na Kazi ya sanaa ikiwa pamoja na nyimbo za aina hiyo kuchezwa kwenye TV kuanzia muda wa saa 6 usiku mpaka saa 12 asubuhi.
Katika mazungumzo yao wameona kuwa kufungia kazi za wasanii sio suluhisho la maadili zaidi wamegundua kwa kufanya hivyo ni kurudisha nyuma sanaa.
-
Video: Diamond apewa ubalozi wa maadili kazi za sanaa
-
Diamond afikia maridhiano na Serikali, ‘maadili kwanza’
Aidha pongezi ziwaendee viongozi wote ambao kwa pamoja wameafikiana kuziachia huru kazi hizo, bila kumsahau Diamond Platinumz ambaye amesimama mbele ya wasanii wote na kulifanikisha jambo ambalo limekuwa kilio kwa wasanii wote wanaotambua mchango mkubwa wa kazi hiyo.
Wizara inahitaji Pongezi Kwa Kuonyesha usikivu na kuona umuhimu na nafasi ya sanaa katika kuliingizia pato taifa letu.
Nyimbo zilizofungiwa na sasa zimeachiwa huru kupigwa kuanzia saa 6 usiku hadi saa 12 asubuhi.