Walimu wa vyuo vikuu wanatarajia kukutana na mwajiri wao leo, Jumamosi kurejesha matumaini ya kumaliza mgomo wa uliodumu kwa muda mrefu.
Mkutano huo unaofanywa na Chama cha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu (Uasu) na Jukwaa la Baraza la Washauri wa Vyuo Vikuu vya Umma (IPUCCF) unatarajiwa kumaliza mgomo uliodumu kwa zaidi ya miezi miwili ambao umezorotesha masomo kuendelea katika vyuo hivyo vya umma.
Wahadhiri wamekabiliwa na shinikizo wakitakiwa kurejea madarasani baada ya vyuo vikuu kadhaa kuzuia mishahara yao.
Baadhi yao wamerejea tayari kazini baada ya kusiani barua za kukubali kuendelea na kazi katika vyuo vikuu wanakofundisha.
Chuo kikuu cha JKUAT ni moja ya chuo ambacho hivi karibuni kimewataka wanafunzi kurejea baada ya vyuo vikuu vingine vikiwemo Moi, Kenyatta, Chuo cha Ufundi Kenya kufanya hivyo kati ya vingine kadhaa.
Mazungumzo hayo yanafanywa chini ya usimamizi wa mkuu wa mazungumzo hayo Isaac Mbeche, ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN).