Uongozi wa Namungo FC umewataka mashabiki wake kuwa watulivu, kufutia tarifa za kuondolewa kwa kocha Hitimana Thiery.

Jana jumatano taarifa za kufukuzwa kwa kocha Hitimana zilichukua nafasi kubwa kwenye  baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, huku kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemedi Suleiman Morocco akitajwa kuchukua nafasi yake.

Katibu Mkuu wa Namungo FC, Ally Suleiman, amesema taarifa rasmi kuondoka ama kubaki kwa kocha Hitimana zitafahamika leo Alhamisi.

“Taarifa rasmi inatarajiwa kutolewa leo na Mwenyekiti wa timu (Hassan Zidadu), ambaye ndiye alitoa amri ya Hitimana kutokwenda na kikosi visiwani Zanzibar, kwa sasa timu iko chini ya Kocha Msaidizi, Gogfrey Okoko,” amesema katibu huyo.

Ameongeza kuwa, katika kuendelea kujiimarisha, timu yao inatarajia kucheza michezo ya ya kirafiki na klabu mojawapo ya Ligi Kuu Zanzibar ambayo wanaamini itawajenga.

Hata hivyo Hitimana amesema sababu kubw aya kubaki jijini Dar es salam ni kutaka kukutana na mwenyekiti wa timu hiyo kwa lengo la kupokea maelekezo.

“Bado sijakutana na mwenyekiti, hivyo sitaweza kuzungumza lolote, kama ni kuhusu kufutwa kazi hilo ni jambo la kawaida kwa kocha yeyote kukabiliana na hali atakayokutana nayo,” amesema Hitimana.

Hitimana ambaye aliipandisha timu hiyo amekuwa na mwanzo mbaya msimu huu wakati msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu Bara aliisaidia klabu hiyo kumaliza nafasi ya tano.

Namungo FC itaikaribisha Al Rabita FC katika mchezo wa kwanza ya michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika Novemba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi jijini Dar es salaam.

Morocco: Sijasaini Namungo FC
Ndayiragije: Taifa Stars ina nafasi, mashabiki msiitupe