Raia nchini Rwanda wanatarajia kupiga kura mapema hii leo kwaajili ya uchaguzi mkuu ambao utaamua hatma ya kiongozi aliyeko madarakani kwa sasa, Paul Kagame na wapinzani wake, Frank Habineza wa chama cha Green Party na Philippe Mpayimana ambaye ni mgombea huru.
Aidha, katika uchaguzi huo mkuu wa Rwanda, vyama vya upinzani nchini humo vimeonekana kutokuwa na nguvu ya kuweza kupambana na Rais wa sasa wa nchi hiyo anayetetea kiti chake, Paul Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa muda mrefu.
Katika uchaguzi huo wapinzani wa Rais wa nchi hiyo wametoa malalamiko kuwa wafuasi wao wamekuwa wakikabiliwa na vitishio, huku uhuru wa demokrasia ukikandamizwa na upande wa chama tawala.
Hata hivyo, Katiba ya nchi hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2015, kwaajili ya kumuongezea muda wa kubaki madarakani Rais wa sasa, Paul Kagame kitu ambacho kilipingwa na wanaharakati, hivyo Katiba hiyo imetoa wigo kwa Rais huyo kubaki madarakani mpaka mwaka 2034.