Shirikisho la Vyama Vya wafanyakazi Nchini, TUCTA, limekutana na baadhi viongozi wa serikali kujadili hatma ya watumishi waliondolewa kazini na Serikali kutokana na vyeti feki .
Ambapo Katibu Mkuu TUCTA, Yahya Msigwa amesema swala hilo limejadiliwa pamoja na viongozi wa serikalini na kufikiwa kwamba maamuzi ya kuwalipa au kutowalipa kifuta jasho watumishi hao yataamriwa mwezi Machi mwaka huu.
-
Majaliwa asimamisha uuzaji wa mali za KNCU
-
JPM afanya uteuzi mwingine Tanesco
-
Video: Onyo la mwisho la JPM, Madudu mazito yaibuliwa Posta
Msigwa amesema Serikali inatambua kuwa watumishi hao wametenda kosa la jinai na la kinidhamu, lakini wataangalia jinsi watakavyoweza kuwaacha.
‘’Baada ya kuishawishi serikali ili watu hao wasiondoke mikoni mitupu, serikali imesema bado mamlaka mbalimbali zinahusika na masuala hayo zinalifanyia kazi suala hilo’’ amesema Msigwa.
Ameongezea kuwa Serikali imsema huenda huenda kbala ya Machi au Aprili mwaka huu kabla ya sherehe za Meoi Mosi itajulikna hatma yao, kama wanaweza kuondoka na kitu kidogo.
Pia amesema wamejadili hoja kuhusiana na ajira kwa walioishia darasa la saba, ambapo serikali iliahidi kuwalipa na kuwarudisha kazini baadhi yao, ifikapo Machi mwaka huu.