Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Khalifa Suleiman amesema kuwa msimamo wa chama hicho ni kutomfukuza Mbunge yeyote ambaye alikuwa upande wa Maalim Seif Hamad na kuongeza kuwa kwa Mbunge atakayeona yuko tayari kuacha ubunge aandike barua ya kujiuzulu.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza juu hatma ya Wabunge ambao walionekana kutounga mkono upande wa Prof. Lipumba wakati wa mgogoro wa chama hicho ukiendelea.

“Katika mahojiano yangu yote yale, tumesema Wabunge hatuna shida nao yoyote ile, ila tumesema tutawaita kama Wabunge ili waje kutoa ushirikiano, na kuhusu Mbunge Katani ambaye alionekana kuwa sio upande wetu hatumfyeki, nachokiamini Katani atatoa ushirikiano, kama anaamini aliingia katika chama ili asipate uongozi basi tunamruhusu kuandika barua ya kujiuzulu Ubunge.”amesema Khalifa.

Hata hivyo, siku za hivi karibuni Khalifa alisema kuwa chama hicho kipo tayari kushirikiana na vyama vingine ikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kujenga demokrasia Tanzania.

Video: Nassari anapaswa kulipa fidia- Wakili Manyama
Mahakama yaridhia uamuzi wa Spika kumvua ubunge Nassari