Klabu ya Soka ya Hausung FC yenye makao yake katika kijiji cha Iboya (Ilowola Sekondari) mkoani Njombe, imefanikiwa kupanda daraja kutoka First League hadi Championship huku ikiwa imesalia na mchezo mmoja mkononi baada ya kufikisha alama 25 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine katika kundi A.

Safari ya Hausung FC ilianzia kwenye Ligi ya Mabingwa wa Mikoa msimu uliopita 2023/24 ambapo ilifanikiwa kupanda First League baada ya kucheza fainali dhidi ya Gunners ya Dodoma ambapo timu zote zilizocheza fainali zilipanda daraja moja kwa moja.
Awali Hausung ilikuwa ikishiriki ligi ya mkoa wa Ruvuma huku makao makuu yake yakiwa ni Songea Mjini na baadae mmiliki wa timu hiyoo Erasto Haule akaamua kuihamishia mkoa wa Njombe ambapo katika msimu wake wa kwanza ikafanikiwa kutwaa Ubingwa wa Mkoa.

Wakati msimu unaanza Hausung FC ilikuwa ikiutumia Uwanja wa Sabasaba Uliopo mjini Njombe lakini mmiliki wa timu hiyo Haule akahamishia timu hiyo Makambako na sasa inatumia uwanja wa Amani kama Uwanja wa Nyumbani.
Katika Mkoa wa Njombe Hausung FC ndiyo timu pekee Inayoshiriki ligi ya Daraja la Juu msimu huu (First League) na msimu ujao (Championship)

Wizara ya Nishati yataja vipaumbele vya Bajeti ya 2025/2026
Chelsea wajuta kumsajili Jadon Sancho