Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hawa Said maarufu kama hawa ntarejea amesema mchoro wa sura ya Diamond aliouchora kifuani kwake, haumaanishi anajipendekeza au anataka kurudiana na staa huyo.

Hawa amesema amesfanya hivyo kama kuonesha shukrani kwa staa huyo kutokana na kujitolea msaada wa matibabu pindi alipokuwa mgonjwa.

Oktoba, 2019 Diamond aliamua kugharamia matibabu ya mwanamuziki huyo kwa kumpeleka India kwaajili ya matatibabu baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo.

Hawa alisema kuwa mchoro huu umeleta maneno mengi kuwa anajibebisha kwa Diamond ili ampende lakini hakuna ukweli wowote kwa aliyomfanyia amekuwa kama kaka yake na anamuheshimu sana.

”Alikuwa mpenzi wangu tukaachana miaka mingi, lakini akathamini urafiki wetu na kuchukua jukumu la kunitibia nitakuwa sina akili nikiwa na mawazo ya kumshawaishi anirudie ilihali amesonga mbele na anamaisha mengine alichonifanyia kinanitosha na nimeamua kuweka kumbukumbu ya hilo mwilini mwangu” alisema Hawa

Ameongeza kuwa mchoro huu umefikisha ujumbe mkubwa kwa Diamond kuliko angesema asante kwa mdomo

 

Video: Bashungwa anadi bidhaa za ndani "tuzipe thamani ziende kimataifa''
Video: Kuolewa kwapasua vichwa, DC, DED watemwa.