Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia amewataka vijana wanaofanya kazi katika Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kilichopo mkoani Mtwara kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa weledi, hivyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia sekta ya gesi.

Ameyasema mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kufanya ziara kwenye miradi mbalimbali ya gesi mkoani Mtwara yenye lengo la kujionea mafanikio na changamoto zake.

Amesema kuwa Serikali imekuwa ikisomesha vijana katika  masuala ya gesi na mafuta, ndani na nje ya nchi lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa sehemu  ya umiliki wa  uchumi wa gesi asilia.

“Vijana wanaofanya kazi nzuri katika kiwanda hiki ni vyema wakahudhuria mafunzo ya mara kwa mara ili kuendana na teknolojia inayobadilika mara kwa mara,”amesema Ghasia

Hata hivyo, katika hatua nyingine, amelishauri  Shirika la Maendeleo ya Petroli  Tanzania (TPDC) kuendelea na mikakati ya kuwa programu za mafunzo ya mara kwa mara kwa wataalam hao kwa kuwa teknolojia inabadilika kila wakati.

 

Polisi wazidi kumng'ang'ania Lissu
Maambukizi ya malaria yapungua nchini