Sakata la watuhumiwa 17 wa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo unyang’anyi, mauaji na uhujumu uchumi, waliotoroka katika mazingira ya kutatanisha limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Kangi Lugola kuibuka mkoani humo.

Lugola amewasimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya, Mkuu wa Kituo cha Polisi na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai wa Wilaya hiyo, na kuagiza askari waliotorokwa na watuhumiwa kukamatwa mara moja.

Waziri Lugola alipowasili mkoani Geita kabla ya kutoa uamuzi huo alifanya kikao na kamati za ulinzi na usalama wilaya na Mkoa, pamoja na kutembelea kituo cha polisi wilaya , Magereza na baadaye eneo ambalo mahabusu hao waliwatoroka.

“Jambo hili limenisikitisha sana, mahali ambapo kuna viongozi wajuu wa polisi, ambapo Maaskari hao wamesababisha tukio hili kana kwamba hakuna kilichotokea, nimeelekeza RPC hao Maaskari hao waliohusika wakamatwe ni waharifu kama waharifu wengine.” amesema Lugola

Hata hivyo, amemtaka Mkuu wa Mkoa huo jambo hilo lazima lichunguzwe kuona kiini chake kwa maelezo waliyoyapata na kwakuwa viongozi hao watatu wamechukua hatua za awali kwa hao Maaskari, ametoa maelekezo kwa Katibu wa Mambo ya Ndani kuwasimamisha kazi OCD, na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Geita.

Polisi anayelinda bungeni auawa nyumbani kwake Nairobi
Uchaguzi Malawi: Rais Mutharika anaongoza

Comments

comments