Jarida la Forbes limetoa orodha ya wana hip hop matajiri zaidi, orodha inayofahamika kwa jina la ‘Hip-Hop Kings List’, ambayo inamuonesha P. Diddy katika nafasi ya kwanza akiingiza dola za kimarekani milioni 60.

Katika orodha hiyo iliyotolewa jana (Septemba 22), P Diddy anaonekana kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kupitia biashara zake anazofanya nje ya muziki ikiwa ni pamoja na Revolt TV, biashara ya nguo zake za ‘Sean John’, biashara ya maji na kinywaji kingine cha ‘Ciroc Vodka’.

Jay Z anashika nafasi ya pili katika orodha hiyo akiwa ameingiza dola milioni 56 ambapo kiasi kikubwa kinatoka kwenye ziara ya muziki ya ‘On The Run’ aliyofanya na mkewe Beyonce Knowles pamoja na kampuni ya Roc Nation.

Hii ni orodha kamili:

  1. P. Diddy – $60 million
  2. Jay-Z – $56 million
  3. Drake – $39 million
  4. Dr. Dre – $33 million
  5. Pharrell Williams – $32 million
  6. Eminem – $31 million
  7. Kanye West – $22 million
  8. Wiz Khalifa – $21.5 million
  9. Nicki Minaj – $21 million
  10. Birdman – $18 million

 

 

Diego Costa Ahukumiwa Kwa Kosa La Kupiga
Lowassa Aukejeli Utafiti Wa Twaweza