Jarida la Forbes limetoa orodha ya wanamuziki wa Hip-Hop walioigiza fedha nyingi kwa mwaka 2017, pesa hizo ni walizoingiza kuanzia mwezi agosti mwaka 2016 hadi agosti 2017.

Sean Combs maarufu kama P Diddy anashika nafasi ya kwanza katika orodha hiyo kwa kulipwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 130, chakushangaza na kikubwa katika list hiyo ni mkongwe Jay Z kushushwa na Drake mpaka nafasi ya tatu. Drake amelipwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 94

Kumekuwa na maingizo mapya wakiwemo msanii Chance the rapper, Dj Khaled, Pitbul, Kendrick Lamar na mkali Wiz Khalifa. Katika orodha hiyo Birdmen ameshika nafasi ya 12 huku Nick Minaj akiwa katika nafasi ya 15 akiwa mwanamke pekee aliyemo katika orodha hiyo ya wanamuziki 20 wa Hip hop wanao ongoza kwa kulipwa fedha nyingi.

Hapa chini ni orodha ya wanamuzi 10 wa Hip hop walioingiza fedha nyingi mwaka 2017;

  1. Diddy – $130 million
  2. Drake – $94 million
  3. Jay Z – $42 million
  4. Dr. Dre – $34.5 million
  5. Chance the Rapper – $33 million
  6. Kendrick Lamar – $30 million
  7. Wiz Khalifa – $28 million
  8. Pitbull – $27 million
  9. DJ Khaled – $24 million
  10. Future – $23 million

 

Aguero apata ajali ya gari
TID atangaza nia ya ubunge 2020, aanza kumwaga sera