Msanii wa bongo fleva, Hawa mayoka maarufu kama hawa ntarejea ameonekana kujutia kukaa nje ya tasnia ya muziki kwa muda mrefu, wakati alipokuwa anasumbuliwa na matatizo ya afya amabpo amesema muziki umekuwa kama vita

Msanii huyo ameeleza hayo alipokuwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni hapa nchini, alipokuwa anatambulisha wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la Shagala Bagala.

Monalisa kuinua vipaji kwa watoto wa kike

“Naona muziki ni vita nina muda mwingi sana nimepoteza kutokuwa kwenye ‘game’, mimi naamini kila mtu ana kitu chake, halafu shabiki zangu lazima nitakuwa nao na sifanyi kwa sababu wengine wanafanya, nisije nikavunjika moyo moja kwa moja maana kila mtu ana nafasi yake” amesema Hawa.

Katika hatua nyingine Hawa amesema kuwa wasitarajie kumuona akirudi kwenye maswala ya pombe na madawa ya kulevya kwa sababu amejiahidi yeye mwenyewe kwamba shetani asimsogelee na kurudi kule alipotoka maana alipotea

Aidha Hawa amesema  huenda asingepitia  matatizo, sasa hivi angekuwa mbali ila anamshukuru Mungu kwa mapito ambayo yamemtokea na anaamini kuna mambo mengine ameyaepuka kutokana na aliyopitia, hata mama yake sasa hivi amependeza na kunawiri sio kama zamani, alivyokuwa na mawazo wakati anasumbuliwa na maradhi.

Vijana watakiwa kutumia michezo kudumisha amani na mshikamano
Video: Rugemalira awasha moto mpya sakata la Escrow, Makombora ya Kikwete yatikisa