Massage ni ukandaji na usuguaji wa sehemu ya mwili kama vile ngozi, tishu, misuli kwa kutumia mikono au mashine maalumu.
Massage (Uchuaji) hutumika kwa tiba mbalimbali za magonjwa hatari ambayo yanaweza kutibika, pia ni tiba kongwe na ya uhakika katika kutibu ila hatari kubwa ni kwamba watu wengi hasa hapa Tanzania huichukulia Massage kwa mtazamo hasi na hii huwafanya wakose hata ufahamu kuwa massage ina umuhimu mkubwa katika miili yao.
Tiba ya massage huleta matokeo chanya pale itakapotolewa na Mtaalamu (Massage Therapist) ambapo magonjwa mbalimbali tangu kale yamekuwa yakitibiwa na bado inaendelea kufanya kazi huku Wataalamu wakifanya tafiti mbalimbali ili kuzidi kuiboresha zaidi.
Massage hutibu magonjwa yafuatayo.
Massage imeonyesha msaada mkubwa sana katika kutibu Magonjwa ya Akili. Massage huamsha seli za ubongo na kuzifanya ziweze kufanya kazi katika hali iliyo nzuri. Hii ni kwa sababu magonjwa mengi ya akili tatizo huwa ni katika seli za ubongo ambazo hushindwa kupokea taarifa vilivyo kutoka katika Milango ya fahamu.
Kansa husababishwa na seli zisizo za kawaida katika mwili. Seli hizi zikiendelea kuwepo huziambukiza seli nyingine na hivyo kuongeza madhara zaidi. Suluhisho pekee ni kuziondoa seli hizo, Kwa sasa kuna Teknolojia ya kuziua Seli hizo zisizo za kawaida ili zisilete madhara zaidi. Massage ni njia bora kabisa ya kuharakisha kuziteketeza seli hizo.Hivyo kwa watu wenye Matatizo hayo ni vema wapate huduma ya massage itawasaidia.
Magonjwa mengi ya Viungo vya mwili yanatibika kiurahisi kupitia Massage kama vile Uvimbe, kukaza kwa misuli, kukaza kwa viungo (joints) ni miongoni mwa Magonjwa yanayoweza kutibika kupitia massage.
Ugonjwa wa kiharusi huu hutokea pale ambapo neva zinazosafirisha taarifa mwilini zinapokufa au kusimama kufanya kazi, Hali hii husababisha kukata kabisa kwa Mawasiliano kati ya Milango ya fahamu na Ubongo. Hivyo husababisha Mtu kushindwa kutumia hata viungo vyake kwa kuwa hakuna tena mawasiliano. Watu wengi wanapopata tatizo hili hukata tama kabisa na kuona kuwa huo ndio mwisho wa Maisha yao.
Magonjwa Mengine yanayotibika kwa Massage ni Msongo wa Mawazo, Simanzi, Maumivu ya Mgongo, na mengineyo.