Wachezaji Hassan Dilunga ‘HD’, Kibu Denis na Criss Mugalu hawatakua sehemu ya Msafara wa Simba SC utakaoondoka kesho Ijumaa (Februari 18) kuelekea Niamey-Niger kwa ajili ya Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya US Gendarmerie.
Mchezo huo wa Mzunguuko wa pili wa Hatua ya ‘Kundi D’ utachezwa mjini Niamey kwenye Uwanja wa Général Seyni Kountché Jumapili (Februari 20), saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Daktari wa timu hiyo, Edwin Anakret amethibitisha kuwa wachezaji hao watatu, watabaki Dar es salaam-Tanzania kufautia kuwa majeruhi.
Amesema Mugalu ameumia kidole atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa Majuma mawili, Dilunga anasumbuliwa na Maumivu wa Mguu na Kibu Denis anauguza jeraha ya Mguu alilolipata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City.
“Mugalu na Dilunga waliumia wakiwa kwenye mazoezi ya kikosi chetu, wote kwa pamoja wanaendelea kuwa nje kwa muda wa majuma matatu, na Kibu Denis matatizo yake yanafahamika tangu alipotolewa kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City.” Amesema Daktari Edwin Anakret.
Katika Msimamo wa ‘Kundi D’ Simba SC ina alama 3 sawa na RS Berkane ya Morocco, huku ASEC Mimosas (Ivory Coast) na US Gendamarie (Niger) zikiwa katika nafasi mbili za mwisho.