Ndoto za mwingereza Heather Watson, kutetea taji la michuano ya kimataifa ya tenisi Hobart, zimefutika baada ya kuchapwa na Johanna Larsson wa Sweden.

Larsson anayeshika nafasi ya 54 kwa ubora duniani upande wa wanawake, alipata ushindi huo licha ya kupoteza seti ya kwanza kwa 3-6 kisha akashinda kwa 6-4 na 6-4.

Hii ilikua ni mchezo wa pili kwa Watson anayeshika nafasi ya 53 kwa ubora duniani, baada ya kumshinda Monica Niculescu, katika mchezo uliopita.

Mchezo huo wa robo fainali ulitumia muda wa saa tatu na dakika kumi na tatu.

Magwiji Wa Tennis Kuanza Na Vibonde Australian open 2016
Rwanda Ipo Tayari Kwa CHAN 2016