Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche (Chadema), amesema kuwa kuna haja ya fedha walizochanga wabunge kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera, zirudishwe bungeni ili ziwasilishwe kwa waathtirika wa tetemeko hilo moja kwa moja .
Amesema kuwa, lengo la wabunge hao kuchanga fedha hizo ni kuwasaidia waathirika hao, ingawa Rais Dkt. Magufuli ameshaagiza fedha zilizochangwa wakati wa tetemeko hilo zitumike kujenga miundo mbinu ya Serikali.
Ameyasema hayo bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu alipokuwa akiomba muongozo kutumia kanuni ya 68 (7),
“Mheshimiwa Naibu Spika, Oktoba 12 mwaka jana, nilisimama hapa na kuomba bunge liahirishe kazi zake kwa ajili ya kujadili tukio la tetemeko la ardhi lililokuwa limetokea Mkoani Kagera Septemba 10 na kubomoa nyumba na mali za watu, jana nimepigiwa simu kule Kagera nikaambiwa mvua zinanyesha na watu bado wanalala nje, naomba mwongozo wa kanuni za bunge ili fedha hizo zirudishwe hapa bungeni wabunge tuzipeleke wenyewe,”
Hata hivyo, Heche amemuomba Naibu Spika kutumia kanuni za bunge ili fedha hizo zirudishwe bungeni na wabunge waweze kuzipeleke wenyewe kwani fedha hizo sio kwa ajili ya kujenga miundo mbinu.