Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche amesema kuwa anawashangaa baadhi ya wasomi wanaosema kuwa Tundu Lissu sio mzalenda huku akisema uzalendo wa nchi si kuiunga mkono Serikali.
Ameyasema hayo baada ya baadhi ya wasomi kuibuka na kuanza kumtuhumu Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, wakisema kuwa kiongozi huyo si mzalendo wa nchi hii wengine wakidai anatumiwa na wazungu kuhujumu nchi
“Leo Benson Bana na wengine wachache wanahoji uzalendo wa Lissu, Bana amewahi kufanya nini cha kizalendo kwa nchi hii? Uzalendo siyo kuunga mkono serikali iliyopo madarakani uzalendo ni kuipenda nchi yako,”amesema Heche
Aidha, amesisitiza kuwa wasomi wa nchi hii wamekuwa wakilitia aibu taifa la Tanzania kutokana na maamuzi yao pamoja na kupotosha ukweli uliowazi na unaoendelea kujitokeza nchini.
-
Zitto Kabwe: Hatukutaka mnunue ndege hovyo hovyo
-
Hamad Rashid: Wanasiasa acheni kutoa kauli za kichochezi
-
Lissu akamatwa na Jeshi la Polisi Dar
Hata hivyo, Heche amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kujitokeza kwa wingi katika mikutano yake ya hadhara ya kusikiliza kero mbalmbali zinazowakabili ili aweze kuona namna ya kuzitatua.