Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (CHADEMA) amesema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi CCM haijawahi kupingana na rushwa kwani rushwa zote zinazofanyika zimeasisiwa na Chama hicho.

Ameyasema hayo mara baada ya TAKUKURU kutupilia mbali ushahidi wa ‘video clip’ iliyowasilishwa ofisini kwao na Wabunge wa CHADEMA, Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki pamoja na Godbless Lema wa Arusha Mjini uliokuwa ukidaiwa kuonyesha madiwani wakipokea rushwa kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Arumeru

Amesema kuwa vita ya rushwa inayozungumzwa na CCM ni vita dhidi ya watu wasiotakiwa na mfumo ndio maana hata kwenye tuhuma za Escrow walikatwa wawili tu japo walitajwa wengi.

“Serikali ya chama cha mapinduzi CCM  haijawahi kupiga vita rushwa na haiwezi kwasababu rushwa zote katika nchi hii zimeasisiwa na zinatokana na CCM, kinachofanyika sasa ni vita dhidi ya watu wasiotakiwa na mfumo, ndio maana hata Escrow waliokamatwa ni wawili lakini bunge lilitaja wengi,”amesema Heche

Hata hivyo, Oktoba 2,  2017 Wabunge Joshua Nassari na Godbless Lema walipeleka ushahidi unaodaiwa kuonyesha kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti akiwashawishi madiwani kutoka mkoani Arusha kupokea rushwa ili waweze kujiuzulu nafasi zao.

JPM: Hiki ni kimbunga vuruga upinzani
Takukuru yatia kapuni ushahidi wa Nassari na Lema