Hatimaye mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania imetoa tamko la kuruhusu matumizi ya helicopter katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu baada ya kuwepo tetesi kuwa mamlaka hiyo imepiga marufuku.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa vyama vinaweza kutumia usafiri huo kusambaza vipeperushi na kuwasafirisha wagombea wake katika maeneo mbalimbali nchini huku ikiwataka kuhakikisha wanachukua tahadhari na kuzingatia taratibu na sheria za matumizi ya anga.

Hivi karibuni, Mamlaka hiyo ilichapisha taarifa kwenye magazeti mbalimbali ikiuelimisha umma juu ya taratibu za matumizi ya usafiri wa anga na jinsi ya kuchukua tahadhari za kiusalama hususani katika kipindi hiki cha uchaguzi ambapo usafiri huo unatarajiwa kutumika kwa wingi zaidi katika kuwafikia wananchi wa maeneo ya pembezoni mwa miji.

NEC Yaingilia Kati Ukawa Kutumia Uwanja Wa Jangwani
Lowassa Aja Na Mbinu Mpya Ya Kampeni Kwa Wanawake