Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Armenia Henrikh Mkhitaryan ametangaza kustaafu soka la kimataifa, baada ya kuitumikia timu ya taifa ya nchi yake katika michezo 95.

Kiungo huyo ambaye aliwahi kutamba na klabu za Borussia Dortmund (2013–2016), Manchester United (2016–2018), Arsenal (2018–2020) na AS Roma anayoichezea hivi sasa anaachama na kikosi cha Armenia huku akiweka Rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika timu hiyo.

Mkhitaryan alikuwa nahodha wa nchi yake amefunga mabao 32, huku akiitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa mwaka 2007.

Ametangaza kustaafu kuichezea timu hiyo kwenye mitandao ya kijamii, akiandika ujumbe alioupa jina, “Kwa heri timu yangu ya taifa pendwa.”

“Nilitaka kushinda kila hatua ya maisha yangu, haijalishi ingekuwa ngumu kiasi gani. Ilikuwa heshima kuchezea taifa langu kwa miaka 15 iliyopita na hata zaidi ya heshima kwa nahodha, kwa miaka sita iliyopita.”

“Baada ya mechi 95 za kimataifa na bidii, nimechukua uamuzi wa kustaafu soka langu la kimataifa na timu ya taifa ya Armenia.”

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 anaamizi maamuzi ya kustaafu soka la kimataifa, yatampa nafasi kubwa ya kuisaidia AS Roma katika Ligi ya Italia ili ifanye vizuri.

Hata hivyo Mkhitaryan anakaribia mwisho wa nyongeza ya mwaka mmoja kwenye mkataba wake na AS Roma na amefanya vyema chini ya Meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho.

Simba SC: Kapombe yuko powa
TASHOKA yajipongeza kufuata kalenda 2022