Meneja wa Kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ Herry Mzozo amethibitisha taarifa za mchezaji wake kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Young Africans.
Akihojiwa na Wasafi FM kupitia kipindi cha Sports Arena leo Jumatano (Desemba 22), Mzozo amesema baada ya mchezaji wake kukamilisha mpango wa kuvunja mkataba na Azam FC jana Jumanne (Desemba 21), amejiunga na Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili.
Amesema kwa sasa kilichobaki kwa mchezaji huyo ni kutambulishwa rasmi na Uongozi wa Young Africans kama mchezaji hali wa klabu hiyo.
“Baada ya kila kitu kukaa sawa kuhusu suala lake ni timu yake ya zamani ya Azam FC kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.”
“Kilichobaki ni kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa Yanga, kila kitu kimekaa sawa.” amesema Mzozo
Sure Boy ameondoka Azam FC aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka 10, baada ya kuingia kwenye matatizo na Uongozi wa klabu hiyo, hali ambayo ilimfanya kusimamishwa kwa muda usiojulikana.