Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Injinia Hersi Said amesema siku zote Uongozi wa klabu hiyo umekuwa ukitamani kutengeneza timu yenye uwezo wa kupata matokeo mazuri wakiwa ugenini katika michuano ya kimataifa.

Young Africans katika mchezo wao wa kwanza wakiwa ugenini dhidi ya Al Merreikh wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 jambo ambalo linawapa urahisi wa kuvuka kwenda hatua ya makundi kwa kuwa mchezo ujao watacheza wakiwa nyumbani.

Kiongozi huyo amesema: “Mara zote sisi kama viongozi tumekuwa tukitamani kupata timu ambayo itaweza kupata matokeo mazuri hata pale timu itakapokuwa inacheza ugenini.

“Tumepata matokeo mazuri Rwanda tukiwa ugenini hii ina maana kubwa sana kwetu kwa kuwa hii timu kubwa nzuri kutoka Sudan na yenye mafanikio makubwa na mazuri.

“Ambacho kipo kwa upande wetu ni kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri pia tukiwa nyumbani ili tuhakikíshe kuwa tunafanikiwa kusonga mbele kwenda katika hatua ya makundi ambapo ndio yalikuwa malengo yetu kwa msimu huu,” amesema kiongozi huyo.

Simba yaichorea ramani Coastal Union
Mashabiki washindwa kumuona Messi