Mgombea kito ya Urais wa klabu ya Young Africans Hersi Said amefungua kampeni zake leo Jumanne (Julai 05), kwa kutangaza hadi nzito ya kujenga Uwanja wa Kaunda.

Hersi anawania kiti cha Urais akiwa Mgombea pekee aliyepitishwa na Kamati ya Utendaji ya Young Africans chini ya Mwenyekiti wake Malangwe Mchungahela.

Mgombea huyo amezungumza na waandishi wa habari na kueleza azma ya kuanza na ujenzi wa Uwanja wa Kaunda uliopo Makao Makuu ya klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Hersi amesema azma hiyo ataanza nayo endapo Wanachama wa Young Africans watampitisha kwenye Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo Julai 09, Jijini Dar es salaam.

“Katika Vipaumbele vikubwa ambavyo nitafanya kama nikipewa nafasi ya Kuwa Rais wa Klabu ya YANGA, ni Kuanzisha Mchakato wa Ujenzi wa Uwanja wa Klabu ambao una uwezo wa Kuingiza Mashabiki Elfu 20”

“Ni Aibu kubwa sana kwa sisi Viongozi kuwa kwenye klabu kubwa yenye mafanikio hapa nchini lakini tunakosa Uwanja wa kufanyia matukio yetu makubwa ya Mechi za Ndani na hata Events ambazo tunataka kufanya na mashabiki zetu.” Amesema Hersi

Uwanja wa Kaunda umekua hautumiki kwa kipindi kitefu kufuatia changamoto za kimazingira, licha ya kujazwa kifusi kwa miaka kadhaa, kufuatia tatizo la kujaa maji wakati wa majira ya Masika.

Selemani Matola afunguka Simba SC
Lourenco kuwakutanisha Thisekedi na Kagame