Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hesabu zinazowasilishwa na CAG kila mwaka si za mashaka bali za uhakika.

Ametoa kauli hiyo leo August 29, 2023 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde, Mohammed Said Issa aliyetaka kujua kama hesabu zinazowasilishwa na CAG kila mwaka ni za mashaka au uhakika.

Amesema, “Hesabu zinazowasilishwa na maafisa masuuli kwa CAG kila mwaka ni za uhakika kwa kuwa zinaandaliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 30 (2) cha Sheria ya Fedha za Umma, SURA 348.”

“Viwango vya kimataifa vya uhasibu katika sekta ya umma (IPSAS); miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara ya Fedha; na mifumo madhubuti ya kielektroniki ya usimamizi wa fedha ikijumuisha mfumo wa uhasibu serikalini (MUSE),” aliongeza Mwigulu.

Aidha, amesema “katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita (2019/20 – 2021/22), taarifa ya CAG imeonesha ongezeko la hati zinazoridhisha kutoka asilimia 92 mpaka 96 kwa serikali kuu; asilimia 70 mpaka 94 kwa serikali za mitaa; na kupungua kutoka asilimia 97 mpaka 98 kwa mashirika na taasisi nyingine za umma.”

Ya Bandari Bunge lilimaliza kazi yake - Spika Tulia
Max Nzengeli afichua siri nzito Young Africans