Bodi ya Mikopo Tanzania imetoa majina ya wanafunzi 15261 walioingia chuo kwa mara ya kwanza, ikiwa ni sehemu (batch) ya tatu ya kutoka majina hayo ya Mikopo.
Akizungumza na Dar24Media Mkurugenzi wa upangaji na utoaji Mikopo katika Bodi ya wanafunzi wa Elimu ya juu Dkt. Veronica Nyahende Amesema kuwa mkopo huo umegharimu kiasi Cha shillingi Bilioni 37.9.
Aidha Mkurugenzi Veronica amewaambia wanafunzi watembelea SIPA ambayo ni akaunti maalum kwaajili ya kupata taarifa zote zinazohusu Mikopo, huku akiwasisitiza kutumika SIPA kwa maana ndo sehemu sahihi yakupata taarifa zao za Mikopo.
Amesema kwa wanafunzi wote walioomba Mikopo kwa batch zote tatu ni wanafunzi 60356, ambapo pesa tayari zimeanza kupelekea vyuoni huku akiwahasa wanafunzi kwenda kwa maafisa Mikopo wa chuo kupata taratibu za Mikopo Yao.