meneja wa muda wa klabu bingwa nchini England, Chelsea,  Guus Hiddink bado hajaridhishwa na na kikosi chake na anadhani itabidi kazi ya ziada ifanyike kuiwezesha timu hiyo kuambulia walau nafasi nne za juu baada ya kufuta ndoto za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Hiddink alisema hayo wakati akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari England baada ya ushindi 3-0 dhidi ya Crystal Palace na kudai kuwa amegundua hivi sasa wana kazi ya kusuka kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao baada ya kufanya vibaya msimu huu.

Hiddink ameteuliwa kwa muda wa miezi sita kuinoa Chelsea akichukua mikoba ya Jose Mourinho aliyetupiwa virago hivi karibuni.

Hata hivyo, kocha huyo akizungumza kwa undani kuhusu mwenendo wa michuano ya Ligi hiyo, alisema hawezi kushangazwa na mafanikio ya klabu zilizopanda daraja msimu huu kufanya vizuri.

Alizitaja baadhi ya timu ambazo zinafanya vizuri kuwa ni Leicester City na Crystal Palace na Watford ambapo alisema wachezaji wake wana ari ya kufanya kazi kwa kuzipa mafanikio timu zao.

Nyundo Ya Magufuli Kuwashukia Wanaotoa Mimba
Koke Aitabiria Mambo Mema Atletico Madrid