Nov 5, Mwaka 2021 msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini Rajabu Abdul Kahali maarufu Harmonize alifanikiwa kutimiza ahadi aliyoiweka kwa mamilioni ya mashabiki wake waliotapakaa sehemu mbali mbali Duniani, zawadi ya ujio wa album mpya ‘HIGH SCHOOL’ yenye jumla ya nyimbo ishirini.
Muda mfupi baada ya album hiyo kutoka, mapokezi makubwa yaliendelea kujidhihirisha ndani ya masaa machache ikiwa ni pamoja na kuchumpa mpaka kwenye namba moja kwenye top albums kupitia digital platforms mbali mbali ikiwamo Apple Music ambako ilizishusha album kadhaa ikiwamo “Only One King” ya Ali Kiba, ‘Equal’ ya Ed sheeran pamoja na Extended playlist ya msanii Rayvanny na kujikita kileleni.
Baada ya album hiyo kutoka kila mmoja amekuwa na mtazamo wake kwenye kuielezea, wengi wakiipongeza na baadhi wakiitoa kasoro album hiyo.
Ukiachana na kuibuka kwa minong’ono kuhusu baadhi ya wasanii wenzie kutomuunga mkono, yapo baadhi ya mambo ambayo wataalamu wa biashara ya muziki wameyatolea ufafanuzi kwa madai ya kuwa pengine Harmonize kuna pahala amekwama kwenye kuifanya album hiyo kufanya vizuri zaidi hasa kwenye upande wa mikakati ya kibiashara na mpangilio mzima wa kuachiwa kwa album hiyo.
Jambo lenye kudhalisha picha ya kuwa pengine mfumo alioutumia unaweza kutoa nafasi kwa wasanii wengine wenye kutarajia kutoa album zao mapema mwaka huu kutumia kasoro hizo kujitengenezea rekodi za kipekee kwenye muziki wao.
Kwani tatizo kubwa la Harmonize ni lipi hasa?
Mchambuzi na mdau wa sanaa ya muziki maarufu mtandaoni kwa jina la Advocate Fi ameibuka na ufafanuzi wa kile alichokiona kama udhaifu katika mchakato na mkakati wa kuiingiza sokoni album hiyo.
“kumekuwa na mitazamo mbalimbali kuhusu project hii. Ni kawaida wengine kuponda na kusifia kazi inapoachiwa kwa mara ya kwanza, sababu watu hupokea kitu emotionally ila siku zote “Truth & time” huthibitisha ubora wa kitu, Binafsi bado nafanya review ya Album hii na kwa ujazo wake ni vigumu kutoa conclusion ya mara moja. Lakini nimejifunza mambo yafuatayo ambayo yamekuwa ni weak point.
- Uwepo tracks nyingi (20 songs) ambazo kwa nature ya Uvivu wa fans wa East Africa inafanya wapoteze focus katika kubainisha ubora wa contents zilizopo. Kulikuwa na uwezekano wa kuwekwa mawe 13 yamoto tu na bado ikakimbiza sokoni.
- Matumizi ya Kingereza kwa wingi inaweza ikafanya watu kuanza kuzielewa tracks zilizomo polepole. Though hii ina faida kwa Fans base ya nje.
- Model ya utambulisho wa Album husika; Binafsi naona kama imeachiwa kienyeji, sidhani kama kulikuwa na uharaka huo ukizingatia Album ni jambo kubwa na ingependeza kama ingefanyika Event fulani na kwa uwepo Harmonzie mwenyewe.
- Ni wakati Harmonize amove on kuhusu Diamond, no matter walifanyia nini huko nyuma ila still Mondy ni Mkubwa kwake na ndio aliyemtoa, he is a godfather to him. Kuna dis tracks unaona kabisa humu anayeimbwa ni nani!! No hatuendi hivyo n it’s for the best.
- Mpangilio “Track Listing” sidhani kama “Sorry” ilipaswa kuanza. Hapa Harmonize kaenda kinyume na Necessity law ya “First impression”.
- Kivuli cha #AfroEast Album kitaendelea kumtafuna yeye binafsi na Artists wengine. Niliwahi kuandika hili huko nyuma kuwa Album yeyote atakayokuja kuitoa itapimwa kwa kipimo kile. Ogopa sana hii kitu.
By Sum up, Still Album ni kali ila kwa anayejua muziki, wale fans fata upepo hopeful watakuja kuielewa taratibu mbele ya safari.” Alisema
Matarajio ya watu wengi ulikuwa nikuona msanii Harmonize anafanya tamasha kubwa la uzinduzi wa album hiyo kama alivyofanya mapema mwaka 2020, wakati wa uzinduzi wa album yake ya kwanza ‘Afro East’, kinyume cha hilo Harmonize aizindua rasmi album hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa instagram (IGTV).